Ruka hadi maudhui

Mfumo wa usimamizi wa famasia Tanzania

Dhibiti stoo. Fuatilia mauzo.Endesha famasia kwa uhakika.

Simamia dawa, mauzo na madeni sehemu moja. Pata tahadhari za dawa zinazokaribia kuisha muda wake, na uone kinachoendelea kwenye famasia yako kupitia simu au kompyuta.

  • Demo: hakuna kujisajili, unatumia data ya mfano.
  • Akaunti mpya: siku 2 za kujaribu bure, hakuna kadi ya benki.

Inatumiwa na famasia zaidi ya 300 Tanzania.

Skrini ya mwanzo ya app ya Famasia kwenye simu: mauzo ya leo, vitendo vya haraka na tahadhari za stoo
Famasia
300+
Mauzo yamerekodiwa
13,500+
Thamani ya mauzo
Tsh 190M+
Dawa zinasimamiwa
8,700+

Takwimu za mfumo, Julai 2026.

Ona mikoa tunakohudumia

Kinachobadilika kwenye famasia yako

Jua dawa zinazopungua na zinazokaribia kuisha muda wake.

Fuatilia kiasi kilichopo na tarehe za mwisho wa matumizi. Pata tahadhari ili upange hatua inayofuata.

Skrini ya Dawa kwenye app ya simu: orodha ya dawa, stoki ndogo na dawa iliyoisha muda

Ona mauzo ya leo, popote ulipo.

Rekodi mauzo na ufuatilie shughuli za famasia kupitia simu au kompyuta.

Skrini ya Rekodi Mauzo kwenye app ya simu: dawa mbili, njia ya malipo na jumla

Fuatilia madeni hadi yalipwe.

Ona salio la kila mteja, rekodi malipo na tuma vikumbusho vya SMS.

SMS hununuliwa kivyake kama salio.

Data ya mfanoUkurasa wa Madeni kwenye demo: wateja wenye madeni na salio lao

Weka majukumu wazi kwa timu yako.

Toa ruhusa kulingana na kazi ya kila mfanyakazi.

Ruhusa za kila jukumu
JukumuMauzoStooMadeniRipotiWafanyakazi
MmilikiNdiyoNdiyoNdiyoNdiyoNdiyo
MsimamiziNdiyoNdiyoNdiyoNdiyoHapana
MfamasiaNdiyoNdiyoNdiyoHapanaHapana
MuuzajiMauzo yake tuHapanaHapanaHapanaHapana
  • Malipo kwa simu na kadi

    Pokea malipo ya M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na kadi kupitia Selcom.

  • Oda za manunuzi

    Tengeneza oda ya manunuzi, itume kwa msambazaji wako kama PDF, kisha pokea stoo ikifika.

  • Muhtasari wa kila siku

    Pata muhtasari wa mauzo, faida na dawa zinazokaribia kuisha kila siku. Unaandaliwa na AI.

Jaribu kabla ya kujisajili.

Demo ni Famasia halisi yenye data ya mfano. Jaribu mambo haya matatu:

  1. Rekodi mauzo ya mfano.
  2. Angalia dawa zinazokaribia kuisha muda wake.
  3. Fungua ripoti ya mauzo.

Data ya demo huwekwa upya mara kwa mara.

Anza kwa hatua tatu.

  1. Fungua akaunti

    Jisajili kwa namba yako ya simu. Hakuna kadi ya benki inayohitajika.

  2. Ingiza stoo yako

    Pakia faili ya Excel, CSV, PDF au picha ya orodha yako. Famasia inaisoma, kisha unakagua kabla ya kuhifadhi.

  3. Anza kuuza

    Rekodi mauzo, fuatilia madeni na uone ripoti popote ulipo.

Bei

Chagua kifurushi kinachofaa famasia yako.

Kila kifurushi kina vipengele vyote. Tofauti ni idadi ya matawi na watumiaji.

Hobby: Tsh 15,500 / mwezi. Premium: Tsh 30,000 / mwezi. Professional: Tsh 50,500 / mwezi. Enterprise: Tsh 102,000 / mwezi

Hobby

Kwa famasia ndogo & ADDO

Tsh 15,500/ mwezi

Jumla Tsh 15,500 kwa mwezi 1

  • Tawi 1
  • Watumiaji 2
Chagua Hobby

Premium

Kwa famasia zinazokua

Tsh 30,000/ mwezi

Jumla Tsh 30,000 kwa mwezi 1

  • Matawi 2
  • Watumiaji 5
Chagua Premium
Tunapendekeza

Professional

Kwa famasia za juu

Tsh 50,500/ mwezi

Jumla Tsh 50,500 kwa mwezi 1

  • Matawi 3
  • Watumiaji 7
Chagua Professional

Enterprise

Kwa minyororo ya famasia

Tsh 102,000/ mwezi

Jumla Tsh 102,000 kwa mwezi 1

  • Matawi bila kikomo
  • Watumiaji bila kikomo
Chagua Enterprise

Kila kifurushi kinajumuisha

  • Stoo, batchi na tahadhari za kuisha muda
  • Mauzo (POS) na risiti
  • Madeni na vikumbusho
  • Oda za manunuzi kwa wasambazaji
  • Ripoti za PDF, Excel na CSV
  • Muhtasari wa kila siku
  • Ruhusa za wafanyakazi
  • App ya simu na kompyuta

Bei ni kwa Shilingi za Tanzania. Jumla kamili huonyeshwa kabla ya kulipa. SMS za vikumbusho hununuliwa kivyake. Printa na vifaa vingine havimo.

Hujui kifurushi kipi kinakufaa?

Ongea nasi WhatsApp

Maswali ya mara kwa mara

Nini ni bure, na kwa muda gani?

Akaunti mpya hupata siku 2 za kujaribu Famasia bure, bila kadi ya benki. Baada ya hapo unachagua kifurushi ili kuendelea kurekodi mauzo. Demo ni bure wakati wote na haihitaji kujisajili. App ya simu ni bure kupakua.

Intaneti ikikatika, nini kinatokea?

Famasia inahitaji intaneti ili kuhifadhi mauzo na stoo. Mtandao ukirudi, unaendelea pale ulipoishia.

Naweza kuingiza orodha yangu ya stoo iliyopo?

Ndiyo. Pakia faili ya Excel, CSV, PDF au picha ya orodha yako. Famasia inaisoma, kisha unakagua na kurekebisha kabla ya kuhifadhi. Ukikwama, tuandikie WhatsApp.

Famasia inafanya kazi kwenye vifaa gani?

Kwenye simu za Android na iPhone, na kwenye kivinjari cha kompyuta. Kwenye simu, kamera inasoma barcode. Risiti huchapishwa kupitia printa iliyounganishwa na kompyuta yako.

Nikihitaji msaada, nawapataje?

Tuandikie WhatsApp au barua pepe hello@famasia.app. Tunapatikana Jumatatu hadi Ijumaa saa 08:00 hadi 18:00, na Jumamosi saa 09:00 hadi 13:00.

Nani anaona nini, na naweza kupakua data yangu?

Kila mfanyakazi huingia kwa namba yake ya simu na PIN, na huona kile tu ambacho ruhusa yake inaruhusu. Ripoti hupakuliwa kwa PDF, Excel au CSV.

Kuna ada nyingine zaidi ya kifurushi?

Hakuna ada ya kuanza. SMS za vikumbusho hununuliwa kivyake kama salio la SMS. Printa na vifaa vingine havimo kwenye bei. Jumla kamili huonyeshwa kabla ya kulipa.

Ona Famasia ikifanya kazi.

Jaribu mauzo, stoo na ripoti kwa data ya mfano. Ukiridhika, fungua akaunti ya famasia yako.

Mikoa 26

Tunahudumia famasia kote Tanzania.

Kutoka Dar es Salaam, Mwanza na Arusha hadi Mtwara. Gusa au chagua mkoa kuona jina lake.

Pakua Famasia

App ya simu ni bure kupakua kwenye iPhone na Android. Kifurushi cha matumizi hulipiwa kivyake. Unaweza pia kutumia Famasia kwenye kivinjari bila kupakua chochote.