Kisheria
Kufuta akaunti na data yako
Unaweza kufuta akaunti yako ya Famasia wakati wowote. Ukurasa huu unaeleza jinsi ya kuomba, nini kinafutwa, na muda gani inachukua.
Imesasishwa mara ya mwisho: 2026-04-20
Njia ya haraka — mipangilio ya akaunti
- Ingia console.famasia.app (au fungua app ya simu).
- Nenda kwenye Mipangilio → Akaunti.
- Bofya “Futa akaunti yangu” kisha thibitisha kwa kuingiza PIN yako.
- Utapokea SMS ya uthibitisho. Bofya kiungo ndani ya saa 24 ili kukamilisha.
Njia ya pili — tuma email
Tuma email hello@famasia.appkutoka anwani iliyosajiliwa Famasia, na ujumbe:
“Ninataka kufuta akaunti yangu ya Famasia na data zote. Namba ya simu iliyosajiliwa: +255…”
Tutathibitisha kupitia SMS au simu ndani ya siku 3 za kazi, kisha tutaendeleza kufuta.
Nini kinafutwa
- Akaunti yako na ya wafanyakazi wako (jina, namba, PIN, picha, historia ya uthibitisho).
- Data ya famasia: dawa, batches, mauzo, madeni, wateja, matumizi, ripoti, mipangilio.
- Picha: logo ya famasia, picha za dawa, picha za profaili, risiti zilizopakiwa.
- Tokeni na vidakuzi: vyote vinavyohusiana na akaunti yako.
- Arifa na SMS historia: DLR, ujumbe uliotumwa, ratiba ya arifa.
Nini kinabaki (na kwa nini)
- Taarifa za malipo (kiasi, tarehe, kitambulisho cha Selcom) — zinahifadhiwa kwa miaka 7 kulingana na sheria za kodi (TRA).
- Logi za usalama zisizotambulishwa(mfano “IP X:Y ilijaribu kuingia”) — hudumu hadi siku 365, kisha zinafutwa kiotomatiki.
Muda
- Siku 1–7: akaunti yako itafungwa mara moja (huwezi kuingia). Data kuu inafutwa kutoka database ya primary.
- Siku 30: data inafutwa kikamilifu kutoka seva zote za Famasia.
- Siku 90: nakala za backup zinafutwa kiotomatiki.
Kabla ya kufuta — hamisha data yako
Tunakushauri kushusha nakala ya data yako kabla ya kufuta:
- Ripoti: tembelea Ripoti na shusha ripoti za mauzo, madeni, na stoo kama PDF au CSV.
- Orodha ya dawa na wateja: tuma email hello@famasia.app kuomba export ya JSON — itatumwa ndani ya siku 7.
Kufuta kifurushi peke yake
Ikiwa unataka kusimamisha kifurushi chako (na kuzuia malipo ya kijielekezi) lakini kuhifadhi akaunti — tembelea Vifurushi→ “Ghairi kifurushi”. Akaunti itabaki hai lakini huwezi kuongeza mauzo mapya baada ya kipindi cha sasa kumalizika.
Wasiliana nasi
Maswali au shida? Tuma email hello@famasia.app. Tutajibu ndani ya siku 3 za kazi.
Una maswali? Tuma email hello@famasia.app au tembelea ukurasa wa msaada.